Monday, April 18, 2016

Baada ya TFDA kufungia Machinjio Vingunguti, Mawaziri wamefika na kutoa maamuzi haya



April 17 2016 Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba aliongozana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mpaka kwenye machinjio ya Vingunguti Dar baada ya machinjio hayo kufungiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kwa kutozingatia usalama na usafi wa maeneo ya machinjio.
Baada ya kikao cha muda mfupi kilichofanyika kwenye machinjio  ya Vingunguti Waziri Nchemba aliyaongea haya ‘Kwanza kuna mambo kadhaa tumeyaona ambayo TFDA wamefanya kazi nzuri sana nawapongeza sana wamebaini ukosefu wa maji, na pia visu vinavyotumika kuchinjia vinasafishwa mahali ambapo sio salama vinasafishwa bafuni‘ >>>Mwigulu Nchemba Waziri wa  Kilimo Uvuvi na Ufugaji
Kwa hiyo nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa nyama itakayokuwa kwenye mabucha itakuwa ni nyama salama lakini tutahakikisha tunaendelea kulinda viwango vya nyama ili wasiweze kupata madhara ya kiafya‘>>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK