Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imelaani vikali hukumu ya kifo aliyopewa mwandishi wa mitandao (blogger) Mohammed Ould Murkatia kwa mdai ya kukengeuka au kuasi dini yake nchini Mauritania
Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya rufaa tarehe 24 mwezi huu , baada ya kusomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza na mahakama mwezi Desemba mwaka jana kutokana na habari aliyoichapisha kwenye blog yake. Kwa mujibu wa ofisi hiyo Murkatia ametubu mara kadhaa lakini haikusaidia kutompa adhabu na kama anavyosisitiza msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville
Wanataka hukumu hiyo itenguliewe
(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)
Tunapenda kusisitiza kwamba chini ya sheria za kimataifa za haki za kijamii na kisiasa ambazo Mauritania iliridhia mwaka 2004, hukumu ya kifo kama bado haifutwa , ingawa tungependa ifutwe, itolewe tuu kwa makossa makubwa. Na tunatumai mahakama kuu nchini Mauritania ambayo sasa inayo kesi hiyo itategua hukumu hiyo ya kifo"
0 maoni:
Post a Comment