Monday, May 9, 2016

GHOROFA LA POROMOKA MOMBASA

Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre, yenye ghorofa sita, iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu.
Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo
Jumba la Nyali Centre huwa na kituo cha mazoezi na mgahawa maarufu
Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi zaidi.
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK