Monday, May 9, 2016

Mafuriko yazua maafa Rwanda




Watu zaidi ya 50 wamefariki na wengine wengi kuachwa bila makao baada ya mvua kubwa kunyesha nchini Rwanda.


Katika baadhi ya maeneo, kumetokea maporomoko ya ardhi.


Mwandishi wa BBC nchini humo Yves Bucyana anasema barabara inayounganisha mji mkuu Kigali na miji ya Musanze na Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda imekuwa haipitiki.



Hasara iliyopatikana kufwatia mafuriko hayo bado ni kubwa kulingana na naibu mkuu wa wilaya ya Gakenke ambayo imeathiriwa sana na mafuriko hayo ni kubwa sana.

Has
ara iliyopatikana kufwatia mafuriko hayo bado ni kubwa kulingana na naibu mkuu wa wilaya ya Gakenke ambayo imeathiriwa sana na mafuriko hayo ni kubwa sana.

Watu 34 walifariki katika eneo hilo la Gakenke, kaskazini mwa Kigali.

Mazishi ya waliofariki yamefanyika leo.

Naibu mkuu wa wilaya ya Gekenke Bi Catherine Uwimana amesisitiza kuna hofu maafa yakawa makubwa zaidi kwa sababu mvua bado inaendelea kunyesha kwa wingi katika eneo hilo.

Mamia kadhaa ya watu wameachwa bila makao na kulingana na afisa huyo watu hao wamejisetiri kwa majirani wakati wakisubiri msaada kutoka wizara husika ambao unatarajiwa kuwasili hivi leo.

Serikali imetuma trekta kuondoa matopo na mchanga ulioziba barabara.

Serikali kupitia wizara inayoshughulikia majanga inasema inatuma msaada wa dharura wa mabati na blanketi kwa mamia ya waathiriwa.

Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika maeneo mengi ya nchi za Afrika Mashariki.
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK