Tuesday, May 17, 2016

Mexico yatakiwa ipige marufuku uvuvi


Shirika la kuhifadhi wa wanyama wa mazingira la World Wildlife Fund, limetoa wito kwa serikali ya Mexico kupiga marufuku uvuvi, katika eneo wanakopatikana aina moja ya nyangumi wanaofahamika kama vaquita porpoises.
Hii ni baada ya idadi ya nyangumi hao kupungua kwa 40% katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Wiki iliyopita, ilitangazwa kuwa ni nyangumi 60 pekee wa aina hiyo waliosalia kote duniani.
Wanyama hao ambao ni waoga, ndio wadogo zaidi katika familia ya nyangumi na wanapatikana katika ghuba ya California.
Nyangumi hao huvuliwa na kuuzwa kimagendo nchini Uchina
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK