Thursday, May 5, 2016

SAFARI YA MATUMAINI YAANZA CONGO DRC

Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii.
Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo 
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK