
Jeshi la wanamaji la Marekani limepiga marufuku unywaji wa pombe kwa wanamaji wote walioko Japan.
Jeshi hilo vilevile limepiga marufuku mwanajeshi yeyote kutoka nje ya kambi zao za kijeshi.
Hatua hiyo imechukuliwa siku moja tu baada ya mwanajeshi Mmarekani kukamatwa na maafisa wa polisi nchini Japan kwa kosa la kuendesha akiwa mlevi katika kisiwa cha Okinawa.
Aimee Mejia, 21, alihusika katika ajali 3 tofauti katika kisiwa hicho na kuwajeruhi vibaya watu wawili.
Jeshi la Marekani lina kambi kubwa katika kisiwa cha Okinawa
Mejia alikuwa akiendesha upande usiofaa wa barabara na akagonga mwanamke mmoja.
Marufuku hiyo ya tembo inaanza kutekelezwa mara moja.
Maafisa watakao ruhusiwa kutoka nje ya kambi ni wale tu watakaopewa vibali maalum na wale watakaokuwa wanatekeleza majukumu muhimu kama ya jeshi na yale ya kifamilia.
Jeshi la Marekani tayari lilikuwa linaomboleza baada ya mfanyikazi wao kubaka na kisha kumuua mwanamke mjapan.

Marekani inatakriban wanamaji 50,000 nchini Japan na 19,000 katika kisiwa hicho na kwa muda sasa wamekuwa wanakabiliwa na shinikizo waondoke kutoka kwa wenyeji.
Waziri mkuu wa Japan bw Shinzo Abe ameelezea kukasirishwa kwake na tukio hilo na hata akalizua katika mkutano na rais Obama ambaye anashiriki katika mkutano wa G7 yaani mataifa 7 yenye nguvu zaidi duniani.
0 maoni:
Post a Comment