Friday, August 19, 2016

Fahamu hii toka kwa Rais MUGABE.

Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ndiye kiongozi mzee zaidi barani Afrika

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefuta ziara yake kwenda nchini Ghana kupokea tuzo la Millennium Lifetime Achievement award, kwa kuliongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika kupata uhuru wake mwaka 1980.

Rais wa Ghana John Mahama alitarajiwa kumpa Mugabe tuzo hiyo, wakati wa warsha ambayo ingefanyika katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ameingoza Zimabawe tangu ipate uhuru na ameapa kusalia madarakani hadi kifo na kukataa wito wa kumtaka ang'atuke. Makubaliano ya uhuru yalitiwa sahihi mwaka 1979 mjini London

Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa safari hiyo, lakini mtandao mmoja nchini Ghana unawanukuu wanadiplomasia nchini Zimbabwe wakisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana masuala ya kisiasa nchini Zimbabwe.

Mabango makubwa yalikuwa yamewekwa mjini Accra kumkaribisha Rais Mugabe na pia hotuba yake ilikuwa imesubiriwa kwa hamu.
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK