Wednesday, September 6, 2017

Viongozi wa CUF wapata ajali wakitokea Dodoma




Stori iliyonifikia asubuhi hii ya Jumatano September 6, 2017 ni kwamba Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi.

Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni watu zaidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
Share:

Thursday, June 8, 2017

Bunge la Seneti kuchapisha ushahidi unaomshutumu Rais Trump


Kamati ya Bunge la Seneti la masuala ya usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi utakaotolewa na mkurugenzi aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais Trump alimtaka mkurugenzi huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama.
James Comey alitoa uchambuzi wa ushaidi wa mazungumzo kati yake na rais Trump aliyofanya naye mara tano wakati Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize na kumheshimu wakati ambapo Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote

Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.
Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria. source BBC.
Share:

Wednesday, May 17, 2017

Rayvanny Atajwa kuwania Tuzo BET Awards2017.

Majina ya wanaowania tuzo za BET 2017 tayari yametoka huku Tanzania ikitajwa kwenye orodha kupitia kwa Mwimbaji wa Bongofleva kutoka kundi la WCB Rayvanny ambaye anawania tuzo kwenye kipengele cha Best International View’s Choices akiwa ni Msanii pekee kutoka Afrika.
Baada ya kuzipokea taarifa hizo Rayvanny alikuwa na haya ya kuwaeleza mashabiki wake.
Share:

Vitu Said Meck Sadiki atavimiss.


Miongoni mwa taarifa zilizotoka kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu May 16, 2017 ni pamoja na JPM kukubali ombi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki kuacha kazi katika nafasi hiyo.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Said Meck Sadiki na kuzungumza naye ambapo amesema moja ya vitu ambavyo atavikumbuka wakati wa utumishi wake ni pamoja na mahusiano yake na waandishi wa habari kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele wakishirikana naye katika kutangaza mafanikio ambayo wananchi huyafurahia.
Aidha, Said Meck Sadiki amebainisha changamoto kubwa ambayo alikabiliana nayo ni pamoja na wakati anahitaji jambo lifanyike, lakini likashindikana hasa katika utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Share:

Thursday, April 13, 2017

Wednesday, April 12, 2017

Thursday, April 6, 2017

TANZANIA YA PANDA HADI NAFASI YA135 KATIKA VIWANGO VYA FIFA


Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kushuka mfululizo katika viwango vya soka dunia vinavyolewa kila baada ya mwisho wa mwezi na FIFA, leo April 6 2017 Tanzania imepokea good news kutoka FIFA baada ya kupanda katika viwango hivyo.
Kwa kawaida viwango vya FIFA hupangwa na shirikisho la soka duniani FIFA kila mwezi kwa kuangalia matokeo ya mechi za kimataifa zilizochezwa na zinazotambuliwa na FIFA katika mwezi husika, Tanzania kwa sasa imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 yaani imepanda kwa nafasi 22.
Katika kipindi cha mwezi March Tanzania imecheza mechi mbili dhidi ya Burundi iliyoshinda kwa goli 2-1 dhidi ya Botswana iliyoshinda kwa goli 2-0, Tanzania wakati inacheza na Burundi ilikuwa nafasi ya 139 na imeshuka hadi nafasi ya 141 wakati Botswana ilikuwa 116 na imeshuka hadi 120.


Share:
Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK