
Mkoa wa Dodoma umetajwa kuwa na viashiria vya juu katika maambukizi ya UKIMWI ikilinganishwa na mikoa mingine. Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa vitu kadhaa vinavyowakutanisha vijana vikiwamo vyuo na sehemu za starehe.
Akizungumza na Gazeti la Mtzanzania, mratibu wa programu za kanda za Afrika,Renatus Kihongo alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012 unaonesha vijana wengi katika manispaa ya Dodoma wanatumia muda mwingi kwenye starehe jambo ambalo ni linatishia uwepo wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Utafiti huo ulifanywa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ‘TACAIDS’ viashiria vya maambukizi ya UKIMWI vipo juu kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu ndio wanaonekana kuwepo katika viashiria hivyo.
Kihongo alisema mkoa wa Dodoma kitaifa upo katika nafasi ya 22 kwa kuwa na maambukizi ya UKIMWI……..>>>’Mara nyingi sehemu yoyote sehemu yoyote yenye maendeleo inakwenda sambamba na viashiria vya maambukizi ya UKIMWI kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu ambao baadaye hujenga uhusiano
Source: MTANZANIA

0 maoni:
Post a Comment