Sunday, December 25, 2016

Ndege yaanguka na wanajeshi 92 nchini Urusi

Ndege ya kijeshi ya Urusi imeanguka huko Black Sea
a
Ndege ya jeshi la Urusi, iliyobeba watu zaidi ya 90, imeanguka katika bahari ya Black Sea , punde baada ya kuondoka Sochi, ikielekea Syria.

Wizara ya Ulinzi inasema hakuna mtu aliyenusurika.

Meli, helikopta, na ndege zisozokuwa na rubani zinaitafuta ndege hiyo. Mabaki ya ndege yamepatikan kilomita moja na nusu kutoka mwambao.

Televisheni ya Urusi imecheza rikodi ya mawasiliano ya mwisho baina ya wanaoongoza safari za ndege ardhini na rubani wa ndege hiyo.Mabaki ya ndege ya Urusi ilioanguka huko Sochi

Hapakuwa na ishara ya matatizo, na rubani alisikika ametulia, hadi ndege ilipotoweka.

Abiria wengi walikuwa kutoka kikundi cha bendi ya muziki cha jeshi kwa jina Alexandrov Ensemble

Wanamuziki hao walitarajiwa kufanya tamasha ya mwaka mpya katika kambi ya Urusi mjini Latakia, Syria.Kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble

Ndege hiyo ilipotea katika mitambo ya Rada, muda mfupi baada ya kupaa angani, kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya Black Sea huko Sochi.
Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK