Thursday, February 2, 2017

RC Makonda atangaza mapya kuhusu biashara ya dawa za kulevya


Leo February 2, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa ya uchunguzi wake kuhusu biashara ya dawa za kulevya kwenye mkoa wake na kuwataja askari 9 wanaotuhumiwa kuhusika au kujihusisha na wafanyabiashara wa dawa hizo.
RC Makonda amezitaka mamlaka za kijeshi kuwaweka chini ya ulinzi askari hao kwa mamlaka yake ili waweze kutoa taarifa kwanini dawa za kulevya bado zinaendelea kuwepo.

Amesema ameyataja baadhi ya maeneo na wamiliki wake ambao wamepewa vibali vya kufanya biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza madawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi February 2, 2017 saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.    

RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi.
Pia  RC Paul Makonda amewataja askari wasiopungua tisa ambao wanatuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya.


Share:

0 maoni:

Post a Comment

Copyright © A star.com All Right Reserve

CONTACT:+255713365518

FACEBOOK